Nimekuwa bubu nimepigwa na butwa Mdomo mzito kinywa kama ndondocha Macho yana magugu sioni mbele najikwa ah Yani ujanja sina nimezorota Naona! Joto si joto baridi si baridi Mwili wa nchoma choma Naona! Kichwa kinawaka moto Moyo unakwenda speed Yani homa si homa, eh! Vipimo nimemaliza kwa manguri daktari Waganga matabibu, he he-eh! Kumbe najilimbikiza maumivu makali Naongeza maswahibu, oh-oh-oh! Nimezunguka kote buza na yombo dovya Sijaaambulia chochote zaidi ya kuchovya chovya Rudi tuishi sote ujinga tu uliniponza Jaribu kusahau yote mtima uje kuupoza Baby, fanya! Turudiane turudiane tena Turudiane tuwe kama zamani Turudiane (fanya turudiane) Turudiane (turudiane) unirudie baby Turudiane (oh-oh) tuwe kama zamani Turudiane Yalopita yamepita si ndwele Rudi tugange yajayo we nimekuzoea Tufanye yamekwisha uje tujenge ya mbele Yale tuachane nayo mwenzako najidodea Rudi tufunike kombe mwanaharamu apite Tusijali tutaonekanaje kwa ndugu jamaa Nimekubali kwako kibonde acha tu nidhalilike Sina habari ata wakisemaje nnachotaka furaha Yale matusi kejeli, vijembe, mafumbo kutupiana Yote tufanye yaishe, eh-eh-eh! Najua twapendana kweli sasa ya nini tunazozana Rudi penzi tudumishee, oh-oh-oh-oh! Nimezunguka kote buza na yombo dovya (nimezunguruka kote) Sijaaambulia chochote zaidi ya kuchovya chovya (oh-oh, oh-oh!) Rudi tuishi sote ujinga tu uliniponza Jaribu kusahau yote mtima uje kuupoza Baby fanya! Turudiane turudiane tena Turudiane tena, unirudie Tuwe kama zamani (iyeeh!) Fanya turudiane (turudiane) Turudiane tena (unirudie baby) Turudiane tuwe kama zamani Turudiane